Ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe leo Mahakama kuu kufuatia kesi aliyoifungua dhidi ya Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda, Kamishna Sirro na ZCO Wambura kwenye sakata la tuhuma za dawa za kulevya. Mahakama kuu leo imetoa maamuzi ambayo Mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu ameyasema yote kwenye hii video hapa chini. ame>
Moja kati ya majina ambayo yamekuwa maarufu ghafla katika upande wa soka ni jina la Kanjunju John shabiki wa Yanga ambaye pia ni mfanyabiashara wa mitumba maeneo ya Karume Dar es Salaam . Kanjunju alikuwa ni miongoni mwa mashabiki wa Yanga waliyoumizwa na Yanga kufungwa goli 2-1 dhidi ya Simba siku ya Jumamosi ya February 25 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam , kwa upande wa Kanjunju aliumia mara mbili kwanza kufungwa timu yake na pili kuliwa mtaji wa nguo wa Tsh 50,000/=. Shilawadu wakimkabidhi Kajunju John hela kutoka kwa Ommy Dimpoz aliyekuwa Marekani Shabiki huyo alibet na kuliwa kutokana na yeye aliweka hela hiyo kuwa Yanga atashinda lakini matokeo yalikuwa tofauti hivyo akapoteza mtaji na kuanza kulia, baada ya hapo msanii Ommy Dimpoz alisikia habari za Kanjunju na kwa huruma yake aliahidi kuwa atampa Tsh 100,000/=.
Comments
Post a Comment