Video | Ukweli kutoka TFF, Ni kweli goli la Kichuya limeua shabiki wa soka?

Jumamosi ya February 25 2017 ilichezwa moja kati ya michezo yenye mvuto na ushindani mkubwa barani Afrika kati ya Simba na Yanga, hii ni moja kati ya Derby kubwa barani Afrika, game ilimalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 2-1. Lakini kuna taarifa ambazo zimesambaa kuwa kuna shabiki wa soka alifariki wakati Shiza Kichuya anaifungia Simba goli la pili.
Uthibitisho umetolewa na shirikisho la soka Tanzania TFF kuhusiana na taarifa hizo, mwenye mamlaka ya kuzitoa habari zote za shirikisho hilo Alfred Lucas ninae katika Exclusive interview.
“Ni kweli tumepata taarifa kwamba kuna shabiki wa mpira wa miguu amefariki kutokana na matokeo ya juzi ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara uliyochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, shabiki huyo ni shabiki wa Simba  na maelezo kutoka kwa mwajiri wake kilichofanya afariki ni bao la pili la Simba”

Comments

Popular posts from this blog