Video | Alisema kama Yanga ikifungwa na Simba anajiuzulu uongozi Yanga, kaamuaje?
- Get link
- X
- Other Apps
Najua utakuwa ni moja kati ya watu wanaotaka kufahamu kuhusiana na ile sauti iliyosambaa mtandaoni ya mjumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga Salum Mkemi kuwa kama Yanga isipoifunga Simba chini ya goli tatu atajiuzulu nafasi yake ya uongozi ndani ya Club ya Yanga.
Kwa bahati mbaya gamu imemalizika kwa Yanga kufungwa goli 2-1 na Simba game iliyochezwa siku ya Jumamosi uwanja wa Taifa Dar es Salaam, AyoTV imempata Salum Mkemi katika exclusive interview, vipi atajiuzulu nafasi yake hiyo ya ujumbe wa kamati ya utendaji kama alivyotoa ahadi?
“Hayo ni maneno ya utani tu kwa hiyo ni masuala ya utani yanakuwepo na yanamalizika, huwezi kusema kiutani eti mwanangu mimi ukifeli nitajiua huo ni utani, Yanga sisi tumepoteza mechi kama tulivyopoteza mechi nyingine tu na tuna nafasi kubwa ya kupata Ubingwa”
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment