Taarifa ya TFDA kuhusu dawa P-500® Paracetamol kuingia Tanzania

Baada ya kuzuka taarifa ya kuingia nchini Dawa aina ya P-500® Paracetamol Tablets IP inayodaiwa kuwa na virusi vya Machupo, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, TFDA ambayo ni Wakala wa Wizara ya Afya wa kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa Tiba nchini imekanusha kuwepo kwa dawa hiyo nchini.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa mamlaka hiyo imeeleza kuwa Dawa hiyo inayotengenezwa na kampuni ya Apex Laboratories Private Limited-Tamil Nadu ya India haijasajiliwa nchini na haipo kwenye soko la Tanzania.
Aidha Mamlaka imewataka Wananchi kutoendelea kusambaza taarifa za uvumi ambazo zina lengo la kuwaogopesha na kuzua taharuki kwa wananchi kabla ya kupata ufafanuzi kutoka mamlaka husika.

Comments

Popular posts from this blog