Timu anayo chezea Mtanzania Mbwana Samatta "KRC Genk" Imetolewa nusu fainali
Usiku wa January 31 2017 mtanzania Mbwana Samatta anayeichezea timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, aliingia uwanjani na kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu yake ya KRC Genk katika mchezo wa nusu fainali ya Croky Cup dhidi ya KV Oostende.
Mchezo huo wa nusu fainali ulichezwa katika uwanja wa nyumbani wa KRC Genk unaojulikana kama Luminus Arena, Genk wamefungwa goli 1-0 na staa wa Zimbabwe Knowledge Musona aliyefunga goli dakika ya 8 ya mchezo, Genk pia wamepata pigo kwa mshambuliaji wao Mbwana Samatta kuumia.
Samatta alicheza hadi dakika ya 24 na kushindwa kuendelea na mchezo, baada ya kuumia na nafasi yake ikachukuliwa na Jose Naranjo aliyekosa penati dakika ya 69, KRC Genk wametolewa katika michuano hiyo lakini bado taarifa zaidi za Samatta zitatolewa baada ya uchunguzi wa majeruhi yake.
Comments
Post a Comment